Entries by Ujenzi Makini

MALIGHAFI YA CHUMA

Sehemu kubwa ya ujenzi wa majengo yanayojengwa kwa mihimili ya chuma hufanyika na aina ya chuma inayoitwa “mild steel” au chuma laini. Hii ni aina ya chuma ambayo ni imara sana. Kwa mfano chuma ya aina hii yenye kipenyo cha wastani wa sentimita 25 mpaka 30 ina uwezo wa kunyanyua au kuning’iniza mzigo wa tani […]

SIFA ZA MALIGHAFI ZA UJENZI

-Kudumu kwa muda mrefu, malighafi za ujenzi zinapaswa kudumu muda mrefu kwa maana ya kwamba hazitakiwi kuwa katika hali ya kushambuliwa kiurahisi na kemikali au aina yoyote ya uharibifu inayoweza kuziletea madhara katika mazingira zilizopo kama vile miale ya jua, unyevu, mvua, kutu, kupauka n.k., -Uimara, malighafi za ujenzi zinapaswa kuweza kuhimili aina zote za […]

MALIGHAFI ZA UJENZI – ZEGE

Tunapozungumzia zege kwenye swala zima la ujenzi huwa tunamaanisha zege lenye chuma ndani yake(reinforced concrete). Kitaalamu inajulikana kama “reinforced cement concrete”, au RCC. RCC ni zege ambayo ndani yake ina nondo au chuma zinazojulikana kama nondo za zege. Huu mchanganyiko wa chuma na zege hufanya kazi vizuri sana na huwa imara sana kwa sababu haivunjiki […]

MFUMO WA PAMPU ZA MAJI ZA ZIMAMOTO.

Kwa kawaida pampu za zimamoto huwekwa kwenye chumba maalumu cha pampu karibu sana na stoo ya mapipa ya maji ya kuzima moto. Pampu zinapaswa kukaa chini ya usawa ya mapipa ya maji ya kuzima moto ili maji yote yaweze kusukumwa kiurahisi kutoka kwenye mapipa wakati wa kuzima moto. Kama ilivyo mifumo mingine kunatakiwa pia kuwe […]

STOO YA MAJI YA ZIMAMOTO(FIRE STORAGE TANKS)

Kiasi cha maji ya zimamoto katika Matangi ya maji ya kuzimia moto kinaamuliwa na kiasi cha hatari ya mradi husika au jengo husika linalolengwa. Kuna Aina Tatu za Viwango vya Hatari za Moto -Hatari ndogo (kama mashule, nyumba za kuishi na maofisi) -Hatari ya kawaida (kama vile viwandani na maofisini) -Hatari kubwa (maeneo yanayohifadhi vitu […]

MIFUMO YA ZIMAMOTO KWENYE JENGO.

-Mifumo ya zimamoto ndio pengine huduma muhimu zaidi katika jengo kwani lengo lake kuu ni kulinda maisha ya watu wanaolitumia jengo na mali zilizopo ndani ya jengo husika. MIFUMO YA ZIMAMOTO IMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU TATU. -Sehemu Ya Kwanza ni mapipa makubwa ya maji yaliyochimbiwa chini ya ardhi au yaliyopo juu ya jengo yanayojulikana kama […]

NAMNA YA KUZUIA MAJI KUVUJA VYOONI NA BAFUNI

Kuna njia kadhaa za kuzuia maji yanayoweza kuvuja vyooni na bafuni lakini hapa tutazungumzia njia kubwa mbili. Kutengeneza “suspending ceiling” yenye urefu wa kama futi moja kuteremeka chini kutoka kwenye sakafu(slab) ya juu ambapo itatengeneza eneo ambalo litawekwa matenki ya maji ya chooni na bafuni kisha kufungiwa vizuri na zege ambali limechanganywa kemikali au karatasi […]